Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Nehemia 1:1 - Swahili Revised Union Version

Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kislevu, mwaka wa ishirini, nilipokuwapo Shushani ngomeni,

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Lifuatalo ni simulizi la Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa, nilipokuwa katika mji mkuu wa Susa, katika mwezi wa Kislevu wa mwaka wa ishirini,

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Lifuatalo ni simulizi la Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa, nilipokuwa katika mji mkuu wa Susa, katika mwezi wa Kislevu wa mwaka wa ishirini,

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Lifuatalo ni simulizi la Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa, nilipokuwa katika mji mkuu wa Susa, katika mwezi wa Kislevu wa mwaka wa ishirini,

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia: Katika mwezi wa Kislevu katika mwaka wa ishirini, wakati nilikuwa ngomeni katika jumba la kifalme la Shushani,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia: Katika mwezi wa Kisleu katika mwaka wa ishirini, wakati nilikuwa ngomeni katika jumba la kifalme la Shushani,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kislevu, mwaka wa ishirini, nilipokuwapo Shushani ngomeni,

Tazama sura
Tafsiri zingine



Nehemia 1:1
9 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo wanaume wote wa Yuda na Benyamini wakakusanyika katika muda wa siku tatu; ulikuwa mwezi wa tisa, siku ya ishirini ya mwezi; na watu wote wakaketi katika uwanja, mbele ya nyumba ya Mungu, wakitetemeka kwa sababu ya neno hilo, na kwa sababu ya mvua kubwa.


Nao wakakwea baadhi ya wana wa Israeli, na wa makuhani, na wa Walawi, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, ili kwenda Yerusalemu, katika mwaka wa saba wa mfalme Artashasta.


Basi hawa ndio waliotia mhuri; Nehemia, ndiye Tirshatha, mwana wa Hakalia, na Sedekia;


Ikawa katika mwezi wa Nisani, mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wowote.


Tena tangu wakati huo nilipowekwa kuwa mtawala wao katika nchi ya Yuda, tangu mwaka wa ishirini hadi mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta mfalme, yaani, miaka kumi na miwili, mimi na ndugu zangu hatukula chakula cha mtawala.


siku zile mfalme Ahasuero alipoketi katika kiti cha enzi cha ufalme wake, huko Susa, mji mkuu ngomeni;


Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa Shushani ukafadhaika.


Nami niliona katika maono; nilipokuwa natazama na nikajionea mwenyewe nikiwa huko Susa, Mji mkuu wa mkoa wa Elamu; nikaona katika maono, nami nilikuwa karibu na mto Ulai.


Ikawa katika mwaka wa nne wa mfalme Dario, neno la BWANA lilimjia Zekaria, siku ya nne ya mwezi wa tisa, yaani, Kislevu.