Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Ezra 7:7 - Swahili Revised Union Version

7 Nao wakakwea baadhi ya wana wa Israeli, na wa makuhani, na wa Walawi, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, ili kwenda Yerusalemu, katika mwaka wa saba wa mfalme Artashasta.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mnamo mwaka wa saba wa utawala wa mfalme Artashasta, Ezra alifunga safari kutoka Babuloni kwenda Yerusalemu. Baadhi ya watu wa Israeli, makuhani, Walawi, waimbaji, walinda malango na wahudumu wa hekalu walikwenda pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mnamo mwaka wa saba wa utawala wa mfalme Artashasta, Ezra alifunga safari kutoka Babuloni kwenda Yerusalemu. Baadhi ya watu wa Israeli, makuhani, Walawi, waimbaji, walinda malango na wahudumu wa hekalu walikwenda pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mnamo mwaka wa saba wa utawala wa mfalme Artashasta, Ezra alifunga safari kutoka Babuloni kwenda Yerusalemu. Baadhi ya watu wa Israeli, makuhani, Walawi, waimbaji, walinda malango na wahudumu wa hekalu walikwenda pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Baadhi ya Waisraeli, wakiwemo makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu na watumishi wa Hekalu, nao walikuja Yerusalemu mwaka wa saba wa utawala wa Mfalme Artashasta.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Pia baadhi ya Waisraeli, wakiwemo makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu na watumishi wa Hekalu, nao walikuja Yerusalemu mwaka wa saba wa utawala wa Mfalme Artashasta.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Nao wakakwea baadhi ya wana wa Israeli, na wa makuhani, na wa Walawi, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, ili kwenda Yerusalemu, katika mwaka wa saba wa mfalme Artashasta.

Tazama sura Nakili

Ezra 7:7
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nao wazee wa Wayahudi wakajenga, wakafanikiwa, kwa msaada wa kuhubiri kwao Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido. Wakajenga, wakaimaliza kazi yao, kwa maagizo ya Mungu wa Israeli, na kwa amri ya Koreshi, na Dario, na Artashasta mfalme wa Uajemi.

Tena tunawaarifu ya kuwa katika habari ya makuhani, na Walawi, na waimbaji, na mabawabu na Wanethini, au watumishi wa nyumba hii ya Mungu, si halali kuwatoza kodi, wala ada, wala ushuru.

Naye Ezra akafika Yerusalemu mwezi wa tano katika mwaka wa saba wa huyo mfalme.

Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kislevu, mwaka wa ishirini, nilipokuwapo Shushani ngomeni,

Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa Torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili;

Basi, hawa ndio makuhani na Walawi waliopanda na Zerubabeli, mwana wa Shealueli, na Yoshua; Seraya, Yeremia, Ezra;

Ikawa katika mwezi wa Nisani, mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wowote.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo