na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, litakuwa kama tini iliyotangulia kuiva kabla ya wakati wa joto, ambayo, aionapo yeye aiangaliaye, huila mara anapoishika mkononi mwake.
Nahumu 3:12 - Swahili Revised Union Version Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva kwanza; ikitikisika zaanguka katika kinywa chake alaye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ngome zako zote ni za tini za mwanzo; zikitikiswa zinamwangukia mlaji kinywani. Biblia Habari Njema - BHND Ngome zako zote ni za tini za mwanzo; zikitikiswa zinamwangukia mlaji kinywani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ngome zako zote ni za tini za mwanzo; zikitikiswa zinamwangukia mlaji kinywani. Neno: Bibilia Takatifu Ngome zako zote ni kama mitini yenye matunda yake ya kwanza yaliyoiva; wakati inapotikiswa, tini huanguka kwenye kinywa chake alaye. Neno: Maandiko Matakatifu Ngome zako zote ni kama mitini yenye matunda yake ya kwanza yaliyoiva; wakati inapotikiswa, tini huanguka kwenye kinywa chake alaye. BIBLIA KISWAHILI Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva kwanza; ikitikisika zaanguka katika kinywa chake alaye. |
na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, litakuwa kama tini iliyotangulia kuiva kabla ya wakati wa joto, ambayo, aionapo yeye aiangaliaye, huila mara anapoishika mkononi mwake.
Kikapu kimoja kilikuwa na tini nzuri sana, kama tini zilizotangulia kuiva; na kikapu cha pili kilikuwa na tini mbovu sana zisizoweza kuliwa, kwa kuwa zilikuwa mbovu sana.
Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana huirundikia udongo, na kuitwaa.
na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.