Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Mwanzo 9:7 - Swahili Revised Union Version Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni kwa wingi, mkaongezeke nchini.” Biblia Habari Njema - BHND Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni kwa wingi, mkaongezeke nchini.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni kwa wingi, mkaongezeke nchini.” Neno: Bibilia Takatifu Bali ninyi, zaeni mwongezeke kwa idadi; zidini duniani na kuijaza.” Neno: Maandiko Matakatifu Kuhusu ninyi, zaeni mwongezeke kwa wingi, mzidi katika dunia na kuijaza.” BIBLIA KISWAHILI Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake. |
Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka katika uzao wako.
Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi.
oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue.