BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
Mwanzo 9:25 - Swahili Revised Union Version Akasema, Na alaaniwe Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema akasema, “Kanaani na alaaniwe! Atakuwa mtumwa wa watumwa kwa ndugu zake.” Biblia Habari Njema - BHND akasema, “Kanaani na alaaniwe! Atakuwa mtumwa wa watumwa kwa ndugu zake.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza akasema, “Kanaani na alaaniwe! Atakuwa mtumwa wa watumwa kwa ndugu zake.” Neno: Bibilia Takatifu akasema, “Alaaniwe Kanaani! Atakuwa mtumwa wa chini kabisa kwa ndugu zake.” Neno: Maandiko Matakatifu akasema, “Alaaniwe Kanaani! Atakuwa mtumwa wa chini sana kuliko watumwa wote kwa ndugu zake.” BIBLIA KISWAHILI Akasema, Na alaaniwe Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake. |
BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kutoka kwa mkono wako;
Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.
Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.
Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, kuongezeka kwa ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.
Basi sasa mmelaaniwa kisha hatakosekana kuwapo mtu wa kwenu aliye mtumwa, wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu.
Siku iyo hiyo Yoshua akawafanya kuwa ni wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano, na kwa ajili ya madhabahu ya BWANA, hata siku hii ya leo, katika mahali hapo atakapopachagua.