Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Mwanzo 8:9 - Swahili Revised Union Version

bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Lakini, kwa vile maji yalikuwa bado yameifunika nchi yote, huyo njiwa hakupata mahali pa kutua, akamrudia Noa katika safina. Noa akanyosha mkono, akamtwaa na kumrudisha ndani ya safina.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Lakini, kwa vile maji yalikuwa bado yameifunika nchi yote, huyo njiwa hakupata mahali pa kutua, akamrudia Noa katika safina. Noa akanyosha mkono, akamtwaa na kumrudisha ndani ya safina.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Lakini, kwa vile maji yalikuwa bado yameifunika nchi yote, huyo njiwa hakupata mahali pa kutua, akamrudia Noa katika safina. Noa akanyosha mkono, akamtwaa na kumrudisha ndani ya safina.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Lakini hua hakupata mahali pa kutua, kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Nuhu ndani ya safina. Nuhu akanyoosha mkono akamchukua yule hua, akamrudisha ndani ya safina.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Lakini hua hakupata mahali pa kutua kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Nuhu ndani ya safina. Nuhu akanyoosha mkono akamchukua yule hua akamrudisha ndani ya safina.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Mwanzo 8:9
8 Marejeleo ya Msalaba  

Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili,

Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi;

Ee nafsi yangu, urudi pumzikoni mwako, Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu.

Ni nani hawa warukao kama wingu, Na kama njiwa waendao madirishani kwao?

Lakini watakaokimbia watakimbia, nao watakuwa juu ya milima kama hua wa bondeni, wote wakilia, kila mmoja katika uovu wake.

Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini BWANA atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika;