Jitengenezee safina ya mti wa mvinje; tengeneza vyumba ukaifunike kwa lami ndani na nje.
Mwanzo 6:15 - Swahili Revised Union Version Hivi ndivyo utakavyoifanya; dhiraa mia tatu urefu wa safina, dhiraa hamsini upana wake, na dhiraa thelathini kwenda juu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utaitengeneza hivi: Urefu wake mita 139, upana wake mita 25 na kimo chake mita 15. Biblia Habari Njema - BHND Utaitengeneza hivi: Urefu wake mita 139, upana wake mita 25 na kimo chake mita 15. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utaitengeneza hivi: urefu wake mita 139, upana wake mita 25 na kimo chake mita 15. Neno: Bibilia Takatifu Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa mia tatu, upana wake dhiraa hamsini, na kimo chake dhiraa thelathini. Neno: Maandiko Matakatifu Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300, upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini. BIBLIA KISWAHILI Hivi ndivyo utakavyoifanya; dhiraa mia tatu urefu wa safina, dhiraa hamsini upana wake, na dhiraa thelathini kwenda juu. |
Jitengenezee safina ya mti wa mvinje; tengeneza vyumba ukaifunike kwa lami ndani na nje.
Uifanyie safina mwangaza, ukaumalize juu kiasi cha mkono mmoja; ukautie mlango wa safina katika ubavu wake; ukaifanyie dari tatu, ya chini, ya pili, na ya tatu.
(Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho kingali kiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni dhiraa tisa, na upana wake dhiraa nane, kwa mfano wa mkono wa mtu).