Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri.
Mwanzo 50:9 - Swahili Revised Union Version Kisha wakaenda pamoja naye wapanda farasi, na magari; wakawa jeshi kubwa sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Pia waliandamana naye wapandafarasi na magari; lilikuwa kundi kubwa sana. Biblia Habari Njema - BHND Pia waliandamana naye wapandafarasi na magari; lilikuwa kundi kubwa sana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Pia waliandamana naye wapandafarasi na magari; lilikuwa kundi kubwa sana. Neno: Bibilia Takatifu Magari ya vita na wapanda farasi pia walipanda pamoja naye. Likawa kundi kubwa sana. Neno: Maandiko Matakatifu Magari makubwa na wapanda farasi pia walipanda pamoja naye. Likawa kundi kubwa sana. BIBLIA KISWAHILI Kisha wakaenda pamoja naye wapanda farasi, na magari; wakawa jeshi kubwa sana. |
Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri.
Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kirefu.
Wakaja mpaka uwanja wa kupuria nafaka wa Atadi, uliyo ng'ambo ya Yordani. Wakaomboleza huko maombolezo makuu, mazito sana. Akafanya matanga ya baba yake siku saba.
Na nyumba yote ya Yusufu, na ndugu zake, na nyumba ya baba yake; wakawaacha watoto wao tu, na kondoo wao, na ng'ombe wao, katika nchi ya Gosheni.
Wawezaje, basi, kurudisha nyuma uso wa ofisa mmoja wa watumishi walio wadogo wa bwana wangu, na kuitumainia Misri upewe magari na farasi?
Nami, tazama, nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu, nao wataingia na kuwafuatia, nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote, kwa magari yake na kwa wapanda farasi wake.
Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.
tena akatwaa magari mia sita yaliyochaguliwa, na magari yote ya Wamisri, na maofisa wa kijeshi juu ya magari hayo yote.