Akakawiakawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi BWANA alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji.
Mwanzo 43:10 - Swahili Revised Union Version maana kama hatungalikawia, hakika tungaliisha kurudi mara ya pili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama tusingalikawia, tungalikuwa tumekwisha kwenda na kurudi mara mbili.” Biblia Habari Njema - BHND Kama tusingalikawia, tungalikuwa tumekwisha kwenda na kurudi mara mbili.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama tusingalikawia, tungalikuwa tumekwisha kwenda na kurudi mara mbili.” Neno: Bibilia Takatifu Hakika, kama hatukuchelewa kuondoka, tungekuwa tumeenda na kurudi mara mbili.” Neno: Maandiko Matakatifu Hakika, kama hatukuchelewa kuondoka, tungekuwa tumekwenda na kurudi mara mbili.” BIBLIA KISWAHILI maana kama hatungalikawia, hakika tungaliisha kurudi mara ya pili. |
Akakawiakawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi BWANA alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji.
Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo zawadi, zeri kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na lozi.
Mimi nitakuwa mdhamini wake, umtake mkononi mwangu. Nisipomleta tena kwako, na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye hatia mbele yako daima;