Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 19:16 - Swahili Revised Union Version

16 Akakawiakawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi BWANA alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Loti akawa anasitasita. Lakini kwa vile Mwenyezi-Mungu alivyomhurumia Loti, wale malaika wakamshika yeye, mkewe na binti zake wawili, wakamtoa nje ya mji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Loti akawa anasitasita. Lakini kwa vile Mwenyezi-Mungu alivyomhurumia Loti, wale malaika wakamshika yeye, mkewe na binti zake wawili, wakamtoa nje ya mji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Loti akawa anasitasita. Lakini kwa vile Mwenyezi-Mungu alivyomhurumia Loti, wale malaika wakamshika yeye, mkewe na binti zake wawili, wakamtoa nje ya mji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Alipositasita, wale wanaume wakamshika mkono wake, na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwahurumia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Alipositasita, wale watu wakamshika mkono wake na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa bwana alikuwa na huruma kwao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Akakawiakawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mikono ya binti zake wawili, kwa jinsi BWANA alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 19:16
39 Marejeleo ya Msalaba  

Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, la sivyo utapotelea katika maangamizi ya mji huu.


maana kama hatungalikawia, hakika tungaliisha kurudi mara ya pili.


Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao.


Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake, Ayadhihirishe matendo yake makuu.


Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu; BWANA ni mwenye fadhili na rehema.


Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Nilifanya haraka wala sikukawia, Kuyatii maagizo yako.


Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiaye BWANA fadhili zitamzunguka.


Tazama, jicho la BWANA li kwao wamchao, Wazingojeao fadhili zake.


Ili kuwaponya nafsi zao kutoka kwa mauti, Na kuwahuisha wakati wa njaa.


Ni nani atamaniye uzima na atakaye kuishi, Siku nyingi afurahie mema?


Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.


Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.


BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;


mwenye kuwaonea huruma watu maelfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.


Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.


Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.


BWANA ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yoyote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne.


Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipigapiga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.


Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenituma; nami nitamfufua siku ya mwisho.


Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.


Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;


kwa kuwa BWANA, Mungu wako, ni Mungu wa rehema; hatakuacha wala kukuangamiza, wala hatalisahau agano la baba zako alilowaapia.


Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.


Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu;


bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kukitimiza kiapo chake alichowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.


si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;


Naye Yoshua akawaambia wale wanaume wawili walioipeleleza nchi, Ingieni katika nyumba ya yule kahaba, mkamtoe huyo mwanamke mwenyewe na vitu vyote alivyo navyo, kama mlivyomwapia.


akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu;


basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo