Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima.
Mwanzo 4:3 - Swahili Revised Union Version Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya muda fulani, Kaini alimtolea Mwenyezi-Mungu sadaka kutokana na mazao ya shambani, Biblia Habari Njema - BHND Baada ya muda fulani, Kaini alimtolea Mwenyezi-Mungu sadaka kutokana na mazao ya shambani, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya muda fulani, Kaini alimtolea Mwenyezi-Mungu sadaka kutokana na mazao ya shambani, Neno: Bibilia Takatifu Baada ya muda, Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba ikiwa sadaka kwa Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwa bwana. BIBLIA KISWAHILI Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. |
Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima.
Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake;
Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi.
Lakini wakati huo wote mimi sikuwako huko Yerusalemu; maana katika mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta, mfalme wa Babeli, nilimrudia mfalme; na baada ya siku kadhaa nikaomba ruhusa tena kwa mfalme.
Yaliyo mazuri katika mafuta, na yaliyo mazuri ya mavuno ya zabibu, na ya mavuno ya nafaka, malimbuko yake watakayompa BWANA, hayo nimekupa wewe.
Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya malipo, nao wameangamia katika maasi ya Kora.