Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani.
Mwanzo 4:20 - Swahili Revised Union Version Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ada alimzaa Yabali ambaye alikuwa baba yao wafugaji waishio mahemani. Biblia Habari Njema - BHND Ada alimzaa Yabali ambaye alikuwa baba yao wafugaji waishio mahemani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ada alimzaa Yabali ambaye alikuwa baba yao wafugaji waishio mahemani. Neno: Bibilia Takatifu Ada akamzaa Yabali; huyu akawa baba wa wale wanaoishi katika mahema na kufuga wanyama. Neno: Maandiko Matakatifu Ada akamzaa Yabali ambaye ni baba wa wale walioishi katika mahema na kufuga wanyama. BIBLIA KISWAHILI Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama. |
Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani.
Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima.
Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa uongo.
Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.