Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri.
Mwanzo 39:1 - Swahili Revised Union Version Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri, naye Potifa, ofisa wa Farao, mkuu wa askari walinzi, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Yosefu alipochukuliwa mpaka Misri, Mmisri mmoja aitwaye Potifa ambaye alikuwa ofisa wa Farao na mkuu wa kikosi chake cha ulinzi, akamnunua kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Yosefu alipochukuliwa mpaka Misri, Mmisri mmoja aitwaye Potifa ambaye alikuwa ofisa wa Farao na mkuu wa kikosi chake cha ulinzi, akamnunua kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Yosefu alipochukuliwa mpaka Misri, Mmisri mmoja aitwaye Potifa ambaye alikuwa ofisa wa Farao na mkuu wa kikosi chake cha ulinzi, akamnunua kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri. Neno: Bibilia Takatifu Wakati huu Yusufu alikuwa amechukuliwa hadi Misri. Mmisri aliyeitwa Potifa, mmoja wa maafisa wa Farao, na aliyekuwa mkuu wa walinzi, akamnunua Yusufu kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati huu Yusufu alikuwa amechukuliwa mpaka Misri. Mmisri aliyeitwa Potifa aliyekuwa mmojawapo wa maafisa wa Farao, mkuu wa ulinzi, akamnunua Yusufu kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri. BIBLIA KISWAHILI Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri, naye Potifa, ofisa wa Farao, mkuu wa askari walinzi, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko. |
Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri.
Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika shimo, wakamuuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
Nao Wamidiani wakamuuza huko Misri, kwa Potifa, mmoja wa maofisa wa Farao, mkuu wa askari walinzi.
Akawatia katika ulinzi nyumbani mwa mkuu wa askari, humo gerezani, mahali alipofungwa Yusufu.
Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri.