Mwanzo 30:10 - Swahili Revised Union Version Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Zilpa akamzalia Yakobo mtoto wa kiume. Biblia Habari Njema - BHND Zilpa akamzalia Yakobo mtoto wa kiume. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Zilpa akamzalia Yakobo mtoto wa kiume. Neno: Bibilia Takatifu Zilpa mjakazi wa Lea akamzalia Yakobo mwana. Neno: Maandiko Matakatifu Mtumishi wa Lea yaani Zilpa, akamzalia Yakobo mwana. BIBLIA KISWAHILI Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana. |
Lea alipoona ya kuwa ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, akampa Yakobo kuwa mkewe.
Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu.
Na mpakani mwa Zabuloni, toka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; Gadi, fungu moja.
Katika wana wa Gadi, kwa kufuata vizazi vyao, jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;
Basi wana wa Reubeni, na hao wana wa Gadi, walikuwa na wanyama wa mifugo wengi sana; nao walipoona nchi ya Yazeri, na nchi ya Gileadi, ya kuwa mahali hapo palikuwa ni mahali pa kuwafaa wanyama;