Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 32:1 - Swahili Revised Union Version

1 Basi wana wa Reubeni, na hao wana wa Gadi, walikuwa na wanyama wa mifugo wengi sana; nao walipoona nchi ya Yazeri, na nchi ya Gileadi, ya kuwa mahali hapo palikuwa ni mahali pa kuwafaa wanyama;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Makabila ya Reubeni na Gadi yalikuwa na mifugo mingi sana. Basi, walipoona kwamba eneo la Yazeri na Gadi lilifaa kwa mifugo,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Makabila ya Reubeni na Gadi yalikuwa na mifugo mingi sana. Basi, walipoona kwamba eneo la Yazeri na Gadi lilifaa kwa mifugo,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Makabila ya Reubeni na Gadi yalikuwa na mifugo mingi sana. Basi, walipoona kwamba eneo la Yazeri na Gadi lilifaa kwa mifugo,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Basi Wareubeni na Wagadi, waliokuwa na makundi makubwa ya ng’ombe, kondoo na mbuzi, waliona kuwa nchi ya Yazeri na nchi ya Gileadi ni nzuri kwa mifugo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kabila la Wareubeni na Wagadi, waliokuwa na makundi makubwa ya ng’ombe, kondoo na mbuzi, waliona kuwa nchi ya Yazeri na nchi ya Gileadi ni nzuri kwa mifugo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Basi wana wa Reubeni, na hao wana wa Gadi, walikuwa na wanyama wa kufugwa wengi sana; nao walipoona nchi ya Yazeri, na nchi ya Gileadi, ya kuwa mahali hapo palikuwa ni mahali pa kuwafaa wanyama;

Tazama sura Nakili




Hesabu 32:1
30 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Abramu alikuwa tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu.


Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng'ombe na kondoo, na hema.


Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa BWANA ameona mateso yangu; sasa mume wangu atanipenda.


Wakamwambia Farao, Tumekuja kukaa ugenini katika nchi hii, kwa sababu wanyama wa watumwa wako hawana malisho, maana njaa ni nzito sana katika nchi ya Kanaani. Basi, twakusihi, uturuhusu sisi watumwa wako tukae katika nchi ya Gosheni.


Wakavuka Yordani, wakapiga kambi huko Aroeri, upande wa kulia wa mji ulioko kati ya bonde la Gadi, na mpaka Yazeri;


kisha wakaja Gileadi, na nchi ya Wahiti huko Kadeshi; kisha wakaja Dani, na kutoka Dani wakazunguka mpaka Sidoni,


Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuziharibu hema zao, pamoja na hao Wameuni waliokuwa wakiishi huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo wao.


Na kundi kubwa la watu waliochangamana mno wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng'ombe, wanyama wengi sana.


Kwa maana BWANA asema hivi, kuhusu habari za nyumba ya mfalme wa Yuda; Wewe u Gileadi kwangu, na kichwa cha Lebanoni; Ila hakika nitakufanya kuwa jangwa, na miji isiyokaliwa na watu.


Nitakulilia, Ee mzabibu wa Sibma, kwa vilio vipitavyo vilio vya Yazeri; matawi yako yalipita juu ya bahari, yalifika hadi bahari ya Yazeri; atekaye nyara ameyaangukia matunda yako ya wakati wa jua, na mavuno yako ya zabibu.


Nami nitamleta Israeli tena malishoni kwake, naye atalisha juu ya Karmeli, na Bashani, na nafsi yake itashiba juu ya milima ya Efraimu, na katika Gileadi.


Je! Hakuna marhamu katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?


Walishe watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao, msituni katikati ya Karmeli; na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale.


Kisha Musa akatuma watu ili kupeleleza Yazeri, nao wakaitwaa miji yake, wakawafukuza Waamori waliokuwamo.


hao wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, wakamwendea Musa na Eleazari kuhani, na wakuu wa mkutano, wakanena nao, wakisema,


Watoto wetu, na wake wetu, na kondoo wetu, na ng'ombe wetu wote, watakuwa hapo katika miji ya Gileadi;


Atarothi, na Diboni, na Yazeri, na Nimra, na Heshboni, na Eleale, na Sebamu, na Nebo na Beoni,


na Atrothi-shofani, na Yazeri, na Yogbeha;


Akajichagulia sehemu ya kwanza, Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria; Akaja pamoja na wakuu wa watu, Akaitekeleza haki ya BWANA, Na hukumu zake kwa Israeli.


Mpaka wao ulikuwa ni Yazeri, na miji hiyo ya Gileadi, na nusu ya nchi ya wana wa Amoni, mpaka Aroeri uliokabili Raba;


Kisha wana wa Israeli wakatuma wajumbe waende kwa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, hadi nchi ya Gileadi; nao ni hawa, Finehasi mwana wa Eleazari kuhani;


Basi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase wakarudi, wakatoka kwa wana wa Israeli katika Shilo, ulioko nchi ya Kanaani, ili waende nchi ya Gileadi, hiyo nchi ya milki yao, waliyokuwa wanaimiliki, sawasawa na amri ya BWANA kwa mkono wa Musa.


Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.


Mbona ulikaa katika mazizi ya kondoo, Kusikiliza filimbi zipigwazo ili kuita makundi? Kwenye vijito vya Reubeni Palikuwa na makusudi makuu mioyoni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo