Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Mwanzo 26:1 - Swahili Revised Union Version

Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Abrahamu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Baadaye palitokea njaa nchini humo, njaa tofauti na ile ya hapo awali wakati wa uhai wa Abrahamu. Isaka akaenda Gerari kwa Abimeleki mfalme wa Wafilisti.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Baadaye palitokea njaa nchini humo, njaa tofauti na ile ya hapo awali wakati wa uhai wa Abrahamu. Isaka akaenda Gerari kwa Abimeleki mfalme wa Wafilisti.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Baadaye palitokea njaa nchini humo, njaa tofauti na ile ya hapo awali wakati wa uhai wa Abrahamu. Isaka akaenda Gerari kwa Abimeleki mfalme wa Wafilisti.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Basi njaa kubwa ikatokea katika nchi hiyo, mbali na njaa iliyotokea wakati wa Ibrahimu. Isaka akaenda kwa Abimeleki mfalme wa Wafilisti huko Gerari.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Basi njaa kubwa ikawa katika nchi hiyo, kuliko ile njaa iliyotangulia iliyotokea wakati wa Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki mfalme wa Wafilisti huko Gerari.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Abrahamu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Mwanzo 26:1
10 Marejeleo ya Msalaba  

Basi kulikuwa na njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa kali katika nchi.

Ikawa, baada ya kufa kwake Abrahamu, Mungu akambariki Isaka mwanawe. Naye Isaka akakaa karibu ya Beer-lahai-roi.

Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.

Wana wa Israeli wakaja wanunue chakula miongoni mwao waliokuja, kwa kuwa kulikuwa na njaa katika nchi ya Kanaani.

Njaa ikawa kali katika nchi.

Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.

BWANA akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii;

Hapo zamani Waamuzi walipokuwa wanatawala, njaa ilitokea katika nchi. Mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaondoka akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili.