Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska.
Mwanzo 22:23 - Swahili Revised Union Version Bethueli akamzaa Rebeka; hao wanane Milka alimzalia Nahori ndugu wa Abrahamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bethueli alimzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori, ndugu yake Abrahamu, watoto hao wanane. Biblia Habari Njema - BHND Bethueli alimzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori, ndugu yake Abrahamu, watoto hao wanane. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bethueli alimzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori, ndugu yake Abrahamu, watoto hao wanane. Neno: Bibilia Takatifu Bethueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori nduguye Ibrahimu hao wana wanane. Neno: Maandiko Matakatifu Bethueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori nduguye Ibrahimu hao wana wanane. BIBLIA KISWAHILI Bethueli akamzaa Rebeka; hao wanane Milka alimzalia Nahori ndugu wa Abrahamu. |
Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska.
Ikawa, kabla hajaisha kunena, tazama, Rebeka anatokea, binti wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu wa Abrahamu, naye ana mtungi begani pake.
Kisha nikamwuliza, U binti wa nani wewe? Naye akasema, Mimi ni binti Bethueli, mwana wa Nahori, Milka aliyemzalia. Nami nikamtia kishaufu puani mwake na vikuku mikononi mwake.
Tazama, huyo Rebeka yuko mbele yako, umchukue, ukaende zako awe mke wa mwana wa bwana wako, kama alivyosema BWANA.
Wakambariki Rebeka, wakamwambia, Dada yetu, wewe uwe mama wa elfu kumi, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mama yake.
Isaka akawa mwenye miaka arubaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.
Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako.
Basi Isaka akamtuma Yakobo, naye akaenda Padan-aramu, kwa Labani, mwana wa Bethueli, Mshami, ndugu wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau.
Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu,