Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.
Mwanzo 16:9 - Swahili Revised Union Version Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bimkubwa wako, ukanyenyekee chini ya mikono yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yule malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Rudi kwa bimkubwa wako Sarai na umtii.” Biblia Habari Njema - BHND Yule malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Rudi kwa bimkubwa wako Sarai na umtii.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yule malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Rudi kwa bimkubwa wako Sarai na umtii.” Neno: Bibilia Takatifu Ndipo malaika wa Mwenyezi Mungu akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.” Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo malaika wa bwana akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.” BIBLIA KISWAHILI Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bimkubwa wako, ukanyenyekee chini ya mikono yake. |
Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.
Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mikononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.
Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, na unakwenda wapi? Akanena, Namkimbia bimkubwa wangu Sarai.
Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako, Usiondoke mara mahali pako ulipo; Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.