BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.
Mwanzo 13:17 - Swahili Revised Union Version Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, inuka uitembelee nchi hii katika mapana na marefu, kwani nitakupa wewe.” Biblia Habari Njema - BHND Basi, inuka uitembelee nchi hii katika mapana na marefu, kwani nitakupa wewe.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, inuka uitembelee nchi hii katika mapana na marefu, kwani nitakupa wewe.” Neno: Bibilia Takatifu Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.” Neno: Maandiko Matakatifu Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.” BIBLIA KISWAHILI Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo. |
BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.
Kisha akamwambia, Mimi ni BWANA, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uimiliki.
Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayokaa kama mgeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Abrahamu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii unayolala nitakupa wewe na uzao wako.
Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.
Lakini BWANA akawahurumia, akawasikitikia, na kuwaangalia, kwa ajili ya agano lake na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, wala hakutaka kuwaangamiza, wala hakuwatupa usoni pake bado.