Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia moja na kumi na tisa, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Mwanzo 11:26 - Swahili Revised Union Version Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tera alipokuwa na umri wa miaka 70, alimzaa Abramu na Nahori na Harani. Biblia Habari Njema - BHND Tera alipokuwa na umri wa miaka 70, alimzaa Abramu na Nahori na Harani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tera alipokuwa na umri wa miaka 70, alimzaa Abramu na Nahori na Harani. Neno: Bibilia Takatifu Tera alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na baadaye akawazaa Nahori na Harani. Neno: Maandiko Matakatifu Tera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani. BIBLIA KISWAHILI Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. |
Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia moja na kumi na tisa, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Kisha huyo mtumishi akatwaa ngamia kumi katika ngamia za bwana wake akaenda zake, maana mali zote za bwana wake zilikuwa mkononi mwake, akaondoka, akaja mpaka Mesopotamia, mpaka mji wa Nahori.
Yoshua akawaambia watu wote, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Baba zenu hapo zamani walikaa ng'ambo ya Mto, maana Tera, baba yake Abrahamu na Nahori; waliitumikia miungu mingine.