Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
Mwanzo 10:8 - Swahili Revised Union Version Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kushi alikuwa baba yake Nimrodi ambaye alikuwa shujaa wa kwanza duniani. Biblia Habari Njema - BHND Kushi alikuwa baba yake Nimrodi ambaye alikuwa shujaa wa kwanza duniani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kushi alikuwa baba yake Nimrodi ambaye alikuwa shujaa wa kwanza duniani. Neno: Bibilia Takatifu Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa shujaa mwenye nguvu duniani. Neno: Maandiko Matakatifu Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani. BIBLIA KISWAHILI Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. |
Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za BWANA.
Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari, Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji. Nendeni, wajumbe wepesi, kwa watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao.
Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake; naye atatuokoa na Mwashuri, atakapoingia katika nchi yetu, na kukanyaga ndani ya mipaka yetu.