Wakafa watu wote waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;
Mwanzo 1:25 - Swahili Revised Union Version Mungu akaumba aina zote za wanyama wa porini na wa kufugwa na viumbe vyote vitambaavyo nchini; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Mungu akafanya aina zote za wanyama wa porini, wanyama wa kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mungu akaona kuwa ni vyema. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Mungu akafanya aina zote za wanyama wa porini, wanyama wa kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mungu akaona kuwa ni vyema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Mungu akafanya aina zote za wanyama wa porini, wanyama wa kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mungu akaona kuwa ni vyema. Neno: Bibilia Takatifu Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, mifugo kulingana na aina zake, na viumbe vyote vinavyotambaa ardhini kulingana na aina zake. Mungu akaona kuwa hili ni jema. Neno: Maandiko Matakatifu Mwenyezi Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, wanyama wa kufugwa kulingana na aina zake, na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi kulingana na aina zake. Mwenyezi Mungu akaona kuwa hili ni jema. BIBLIA KISWAHILI Mungu akaumba aina zote za wanyama wa porini na wa kufugwa na viumbe vyote vitambaavyo juu ya nchi; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. |
Wakafa watu wote waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;
kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu.
Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha; Na ndege wa angani, nao watakuambia;
Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio katika nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo.