Nawe utasema, Bwana MUNGU asema hivi; Mji umwagao damu ndani yake, ili wakati wake upate kuja; mji ufanyao vinyago juu ya nafsi yake, ili ujitie unajisi!
Mika 3:10 - Swahili Revised Union Version Wanaoijenga Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyinyi mnajenga mji wa Siyoni kwa damu, naam, mji wa Yerusalemu kwa dhuluma. Biblia Habari Njema - BHND Nyinyi mnajenga mji wa Siyoni kwa damu, naam, mji wa Yerusalemu kwa dhuluma. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyinyi mnajenga mji wa Siyoni kwa damu, naam, mji wa Yerusalemu kwa dhuluma. Neno: Bibilia Takatifu mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu na Yerusalemu kwa uovu. Neno: Maandiko Matakatifu mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu na Yerusalemu kwa uovu. BIBLIA KISWAHILI Wanaoijenga Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu. |
Nawe utasema, Bwana MUNGU asema hivi; Mji umwagao damu ndani yake, ili wakati wake upate kuja; mji ufanyao vinyago juu ya nafsi yake, ili ujitie unajisi!
Mtu amchaye Mungu ametoweka, asionekane katika nchi, wala hapana mtu mwenye adili katika wanadamu; wote huotea ili kumwaga damu; kila mtu humwinda ndugu yake kwa wavu.
Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; mahakimu wake ni mbwamwitu wa jioni; wasiobakiza kitu chochote mpaka asubuhi.
wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima.