Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa joto, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
Mhubiri 1:5 - Swahili Revised Union Version Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jua lachomoza na kutua; laharakisha kwenda machweoni. Biblia Habari Njema - BHND Jua lachomoza na kutua; laharakisha kwenda machweoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jua lachomoza na kutua; laharakisha kwenda machweoni. Neno: Bibilia Takatifu Jua huchomoza na jua huzama, nalo huharakisha kurudi mawioni. Neno: Maandiko Matakatifu Jua huchomoza na jua huzama, nalo huharakisha kurudi mawioni. BIBLIA KISWAHILI Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa mawio yake. |
Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa joto, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
BWANA asema hivi, Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana, na agano langu la usiku, hata usiwepo tena mchana na usiku kwa wakati wake,
Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.