Naye Yusufu alipomwona Benyamini pamoja nao, akamwambia msimamizi wa nyumba yake, Uwalete watu hawa nyumbani, ukachinje mnyama na kuwaandalia, maana watu hawa watakula pamoja nami adhuhuri.
Methali 9:2 - Swahili Revised Union Version Amechinja nyama zake, amechanganya divai yake, Ameiandalia meza yake pia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amechinja wanyama wa karamu, divai yake ameitayarisha, ametandika meza yake. Biblia Habari Njema - BHND Amechinja wanyama wa karamu, divai yake ameitayarisha, ametandika meza yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amechinja wanyama wa karamu, divai yake ameitayarisha, ametandika meza yake. Neno: Bibilia Takatifu Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake; pia ameandaa meza yake. Neno: Maandiko Matakatifu Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake; pia ameandaa meza yake. BIBLIA KISWAHILI Amechinja nyama zake, amechanganya divai yake, Ameiandalia meza yake pia. |
Naye Yusufu alipomwona Benyamini pamoja nao, akamwambia msimamizi wa nyumba yake, Uwalete watu hawa nyumbani, ukachinje mnyama na kuwaandalia, maana watu hawa watakula pamoja nami adhuhuri.
Ningekuongoza nyumbani mwa mamangu, Naye angenifundisha; Ningekunywesha divai iliyokolea, Divai mpya ya mkomamanga wangu.
Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.