Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
Methali 9:10 - Swahili Revised Union Version Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima; na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili. Biblia Habari Njema - BHND Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima; na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima; na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili. Neno: Bibilia Takatifu “Kumcha Mwenyezi Mungu ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu. Neno: Maandiko Matakatifu “Kumcha bwana ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu. BIBLIA KISWAHILI Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu. |
Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.
Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri, Sifa zake zadumu milele.
Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Nasi tunajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.