Methali 4:27 - Swahili Revised Union Version Usigeuke kwa kulia wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usigeukie kulia wala kushoto; epusha mguu wako mbali na uovu. Biblia Habari Njema - BHND Usigeukie kulia wala kushoto; epusha mguu wako mbali na uovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usigeukie kulia wala kushoto; epusha mguu wako mbali na uovu. Neno: Bibilia Takatifu Usigeuke kulia wala kushoto; epusha mguu wako na ubaya. Neno: Maandiko Matakatifu Usigeuke kulia wala kushoto; epusha mguu wako na ubaya. BIBLIA KISWAHILI Usigeuke kulia wala kushoto; Ondoa mguu wako maovuni. |
Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.
Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lolote, kwenda mkono wa kulia wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na BWANA, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kulia wala wa kushoto.
Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda kulingana na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kulia, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.