Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
Methali 4:2 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana ninawapa maagizo mema, msiyakatae mafundisho yangu. Biblia Habari Njema - BHND Maana ninawapa maagizo mema, msiyakatae mafundisho yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana ninawapa maagizo mema, msiyakatae mafundisho yangu. Neno: Bibilia Takatifu Ninawapa mafundisho ya maana, kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu. Neno: Maandiko Matakatifu Ninawapa mafundisho ya maana, kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu. |
Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu;
Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu; Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.
Nasi tumeitii sauti ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, katika yote aliyotuamuru, kwamba tusinywe divai siku zetu zote, sisi, na wake zetu, na wana wetu, na binti zetu;
Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea.
Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoefu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.
akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.