Lakini Farao alipoona ya kuwa pana nafuu, akaufanya moyo wake kuwa mzito, asiwasikize; kama BWANA alivyonena.
Methali 26:11 - Swahili Revised Union Version Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake, ni kama mbwa anayekula matapishi yake. Biblia Habari Njema - BHND Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake, ni kama mbwa anayekula matapishi yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake, ni kama mbwa anayekula matapishi yake. Neno: Bibilia Takatifu Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake, ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake. Neno: Maandiko Matakatifu Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake, ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake. BIBLIA KISWAHILI Kama vile mbwa arudiavyo matapishi yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena. |
Lakini Farao alipoona ya kuwa pana nafuu, akaufanya moyo wake kuwa mzito, asiwasikize; kama BWANA alivyonena.
Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Fundi stadi hufanyiza vitu vyote; Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao.
Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaagaa matopeni.