Jina lako na litukuzwe milele, kwa kusema, BWANA wa majeshi ndiye Mungu juu ya Israeli; na nyumba ya mtumishi wako, Daudi, itaimarika mbele zako.
Methali 24:3 - Swahili Revised Union Version Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyumba hujengwa kwa hekima, na kuimarishwa kwa busara. Biblia Habari Njema - BHND Nyumba hujengwa kwa hekima, na kuimarishwa kwa busara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyumba hujengwa kwa hekima, na kuimarishwa kwa busara. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kupitia ufahamu huimarishwa; Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa BIBLIA KISWAHILI Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, |
Jina lako na litukuzwe milele, kwa kusema, BWANA wa majeshi ndiye Mungu juu ya Israeli; na nyumba ya mtumishi wako, Daudi, itaimarika mbele zako.
Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.
Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani.