Methali 23:32 - Swahili Revised Union Version Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwishowe huuma kama nyoka; huchoma kama nyoka mwenye sumu. Biblia Habari Njema - BHND Mwishowe huuma kama nyoka; huchoma kama nyoka mwenye sumu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwishowe huuma kama nyoka; huchoma kama nyoka mwenye sumu. Neno: Bibilia Takatifu Mwishowe huuma kama nyoka na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu. Neno: Maandiko Matakatifu Mwishowe huuma kama nyoka na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu. BIBLIA KISWAHILI Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. |
Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao.
Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa kunyonya atatia mkono wake katika pango la fira.
Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.
Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?
Maana, tazama, nitatuma nyoka, naam, fira, kati yenu, wasioweza kutumbuizwa kwa uganga; nao watawauma, asema BWANA.
Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
Nao wajapojificha katika kilele cha Karmeli, nitawatafuta na kuwatoa toka huko; na wajapositirika katika vilindi vya bahari nisiwaone, nitamwagiza joka huko, naye atawauma.
Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.