Methali 23:10 - Swahili Revised Union Version Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani; Wala usiingie katika mashamba ya yatima; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usiondoe alama ya mpaka wa zamani, wala usiingilie mashamba ya yatima, Biblia Habari Njema - BHND Usiondoe alama ya mpaka wa zamani, wala usiingilie mashamba ya yatima, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usiondoe alama ya mpaka wa zamani, wala usiingilie mashamba ya yatima, Neno: Bibilia Takatifu Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima, Neno: Maandiko Matakatifu Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima, BIBLIA KISWAHILI Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani; Wala usiingie katika mashamba ya yatima; |
BWANA asema hivi, Fanyeni hukumu na haki, mkamtoe yeye aliyetekwa katika mikono ya mdhalimu; wala msiwatende mabaya mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kuwadhulumu, wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia katika mahali hapa.
Maana kama mkitengeneza kabisa njia zenu na matendo yenu; kama mkihukumu hukumu ya haki kati ya mtu na jirani yake;
kama hamwonei mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, wala kuifuata miungu mingine kwa hasara yenu wenyewe;
tena msimdhulumu mjane, wala yatima, wala mgeni, wala maskini; wala mtu awaye yote miongoni mwenu asiwaze mabaya juu ya ndugu yake moyoni mwake.
Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.
Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki.
Dini iliyo safi, isiyo na dosari mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.