Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Methali 22:16 - Swahili Revised Union Version Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayemdhulumu maskini atamfanya afaidike mwishowe, anayewapa matajiri zawadi ataishia kuwa maskini. Biblia Habari Njema - BHND Anayemdhulumu maskini atamfanya afaidike mwishowe, anayewapa matajiri zawadi ataishia kuwa maskini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayemdhulumu maskini atamfanya afaidike mwishowe, anayewapa matajiri zawadi ataishia kuwa maskini. Neno: Bibilia Takatifu Yeye anayemdhulumu maskini ili kujiongezea mali, naye anayempa tajiri zawadi, wote huwa maskini. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye amwoneaye maskini ili kujiongezea mali, naye ampaye tajiri zawadi, wote huwa maskini. BIBLIA KISWAHILI Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara. |
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye Juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao.
Akalia, akasema, Ee baba Abrahamu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, aupoze ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.