Methali 20:12 - Swahili Revised Union Version Sikio lisikialo, na jicho lionalo, BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikio lisikialo na jicho lionalo, yote mawili kayafanya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Sikio lisikialo na jicho lionalo, yote mawili kayafanya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikio lisikialo na jicho lionalo, yote mawili kayafanya Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Masikio yasikiayo na macho yaonayo: Mwenyezi Mungu ndiye alivifanya vyote viwili. Neno: Maandiko Matakatifu Masikio yasikiayo na macho yaonayo, bwana ndiye alivifanya vyote viwili. BIBLIA KISWAHILI Sikio lisikialo, na jicho lionalo, BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili. |
BWANA akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, BWANA?
Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.
Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho kitabu, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.
uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.