Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.
Methali 2:21 - Swahili Revised Union Version Maana wanyofu watakaa katika nchi, Na wakamilifu watadumu ndani yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana wanyofu wataipata nchi, na waaminifu watadumu ndani yake. Biblia Habari Njema - BHND Maana wanyofu wataipata nchi, na waaminifu watadumu ndani yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana wanyofu wataipata nchi, na waaminifu watadumu ndani yake. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi, nao wasio na lawama watabakia ndani yake. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi, nao wasio na lawama watabakia ndani yake. BIBLIA KISWAHILI Maana wanyofu watakaa katika nchi, Na wakamilifu watadumu ndani yake. |
Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.
Basi hivyo BWANA akaubariki huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu moja, na punda wake elfu moja.
Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema.