Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.
Methali 2:19 - Swahili Revised Union Version Katika hao wamwendeao harudi hata mmoja, Wala hawazifikilii njia za uzima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeyote amwendeaye kamwe harudi, wala hairudii tena njia ya uhai. Biblia Habari Njema - BHND Yeyote amwendeaye kamwe harudi, wala hairudii tena njia ya uhai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeyote amwendeaye kamwe harudi, wala hairudii tena njia ya uhai. Neno: Bibilia Takatifu Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi, au kufikia mapito ya uzima. Neno: Maandiko Matakatifu Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi, au kufikia mapito ya uzima. BIBLIA KISWAHILI Katika hao wamwendeao harudi hata mmoja, Wala hawazifikilii njia za uzima. |
Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.
Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye.
Je! Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoadoa yake? Kama aweza, ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya.
Sitawaadhibu binti zenu wazinipo, wala bibi arusi zenu wafanyapo uasherati; maana wenyewe huenda kando pamoja na wanawake wazinzi, hutoa dhabihu pamoja na makahaba; na watu hawa wasiofahamu wataangamia.
ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;