Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.
Methali 2:15 - Swahili Revised Union Version Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema watu ambao mienendo yao imepotoka, nazo njia zao haziaminiki. Biblia Habari Njema - BHND watu ambao mienendo yao imepotoka, nazo njia zao haziaminiki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza watu ambao mienendo yao imepotoka, nazo njia zao haziaminiki. Neno: Bibilia Takatifu ambao mapito yao yamepotoka, na ambao ni wapotovu katika njia zao. Neno: Maandiko Matakatifu ambao mapito yao yamepotoka na ambao ni wapotovu katika njia zao. BIBLIA KISWAHILI Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao. |
Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.
Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau.
Njia yake aliyelemewa na dhambi imepotoka sana; Bali mtu aliye safi, kazi yake ni sawasawa.
Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika mienendo yao; wamejifanyia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani.
Wametenda mambo ya uharibifu, Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao; Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka.
mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,