Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la BWANA, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.
Methali 19:5 - Swahili Revised Union Version Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shahidi mwongo hataacha kuadhibiwa; asemaye uongo hataepa adhabu. Biblia Habari Njema - BHND Shahidi mwongo hataacha kuadhibiwa; asemaye uongo hataepa adhabu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shahidi mwongo hataacha kuadhibiwa; asemaye uongo hataepa adhabu. Neno: Bibilia Takatifu Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo hataachwa huru. Neno: Maandiko Matakatifu Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo hataachwa huru. BIBLIA KISWAHILI Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka. |
Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la BWANA, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.
Basi kwa hiyo usimwachilie, kwa kuwa wewe u mtu wa akili; nawe utajua ikupasayo umtendee, na mvi zake utazishusha Ahera pamoja na damu.
Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.
Usilitaje bure Jina la BWANA, Mungu wako; maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia, mtu alitajaye jina lake bure.