Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko.
Methali 10:7 - Swahili Revised Union Version Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka; Bali jina la mtu mwovu litaoza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waadilifu hukumbukwa kwa baraka, lakini waovu watasahaulika kabisa. Biblia Habari Njema - BHND Waadilifu hukumbukwa kwa baraka, lakini waovu watasahaulika kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waadilifu hukumbukwa kwa baraka, lakini waovu watasahaulika kabisa. Neno: Bibilia Takatifu Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, lakini jina la mwovu litaoza. Neno: Maandiko Matakatifu Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, lakini jina la mwovu litaoza. BIBLIA KISWAHILI Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka; Bali jina la mtu mwovu litaoza. |
Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko.
Maana nitaulinda mji huu, niuokoe, kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.
Wakamzika katika mji wa Daudi kati ya wafalme, kwa sababu ametenda mema katika Israeli, na kwa Mungu, na katika nyumba yake.
Hezekia akalala na babaze, wakamzika mahali pa kupandia makaburi ya wana wa Daudi; nao Yuda wote na wenyeji wa Yerusalemu wakamfanyia heshima alipokufa. Na Manase mwanawe akatawala mahali pake.
Tumbo lililomzaa litamsahau; buu litamla na kuona tamu; Hatakumbukwa tena; Na udhalimu utavunjwa kama mti.
Pia nikaona waovu wamezikwa, nao wamefika kaburini; tena waliofanya mema wameondoka katika patakatifu, nao wamesahauliwa mjini. Hayo nayo ni ubatili.
Nami nitainuka, nishindane nao; asema BWANA wa majeshi; na katika Babeli nitang'oa jina na mabaki, mwana na mjukuu; asema BWANA.
Ee BWANA, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha BWANA, kisima cha maji yaliyo hai.
Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.
Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;