Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 14:22 - Swahili Revised Union Version

22 Nami nitainuka, nishindane nao; asema BWANA wa majeshi; na katika Babeli nitang'oa jina na mabaki, mwana na mjukuu; asema BWANA.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Nitaushambulia mji wa Babuloni na kuuangamiza kabisa. Nitaharibu kila kitu, mji wote, watoto na yeyote aliyebaki hai. Mimi Mwenyezi-Mungu nimenena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Nitaushambulia mji wa Babuloni na kuuangamiza kabisa. Nitaharibu kila kitu, mji wote, watoto na yeyote aliyebaki hai. Mimi Mwenyezi-Mungu nimenena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Nitaushambulia mji wa Babuloni na kuuangamiza kabisa. Nitaharibu kila kitu, mji wote, watoto na yeyote aliyebaki hai. Mimi Mwenyezi-Mungu nimenena.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni asema, “Nitainuka dhidi yao, nitalikatilia mbali jina lake kutoka Babeli pamoja na watu wake walionusurika, watoto wake na wazao wake,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 bwana Mwenye Nguvu Zote asema, “Nitainuka dhidi yao, nitalikatilia mbali jina lake kutoka Babeli pamoja na watu wake walionusurika, watoto wake na wazao wake,” asema bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

22 Nami nitainuka, nishindane nao; asema BWANA wa majeshi; na katika Babeli nitang'oa jina na mabaki, mwana na mjukuu; asema BWANA.

Tazama sura Nakili

Isaya 14:22
15 Marejeleo ya Msalaba  

tazama, kwa hiyo mimi nitaleta mabaya juu ya nyumba yake Yeroboamu, nami nitakatilia mbali kutoka kwa Yeroboamu kila mwanamume, aliyefungwa na aliyeachwa katika Israeli, nami kuondoa nitawaondoa waliobaki wa nyumba yake Yeroboamu, kama mtu aondoavyo mavi, hata itakapokwisha pia.

Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.

Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka; Bali jina la mtu mwovu litaoza.

watu waliotoka katika nchi iliyo mbali, tokea upande wa mwisho wa mbingu; naam, BWANA na silaha za ghadhabu yake, ili aiangamize nchi yote.

Na, tazama, linakuja kundi la watu, wapanda farasi, wakienda wawili wawili. Akajibu na kusema, Babeli umeanguka, umeanguka; na sanamu zote za miungu yake zimevunjwa chini.

BWANA, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Kwa ajili yenu nimetuma ujumbe Babeli nami nitawashusha wote mfano wa wakimbizi, naam, Wakaldayo, katika merikebu zao walizozifurahia.

Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hakuna mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia.

Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asiwepo tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo