Basi Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha Daudi baba yake; na ufalme wake ukawa imara sana.
Methali 1:1 - Swahili Revised Union Version Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hizi ni methali za Solomoni mfalme wa Israeli, mwana wa Daudi. Biblia Habari Njema - BHND Hizi ni methali za Solomoni mfalme wa Israeli, mwana wa Daudi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hizi ni methali za Solomoni mfalme wa Israeli, mwana wa Daudi. Neno: Bibilia Takatifu Mithali za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli: Neno: Maandiko Matakatifu Mithali za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli: BIBLIA KISWAHILI Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli. |
Basi Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha Daudi baba yake; na ufalme wake ukawa imara sana.
BWANA akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidia. Ikawa amani kati yao Hiramu na Sulemani; wakafanya mikataba kati yao wawili.
tazama, utapata mwana, atakayekuwa mtu wa amani; nami nitampa amani mbele ya adui zake pande zote; kwani jina lake litakuwa Sulemani, nami nitawapa Israeli amani na utulivu siku zake;
tena katika wana wangu wote (kwani BWANA amenipa wana wengi), amemchagua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA, juu ya Israeli.
Ndipo Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha BWANA, awe mfalme badala ya Daudi babaye, akafanikiwa; nao Israeli wote wakamtii.
Akafa akiwa mzee sana, mwenye maisha marefu, mali na heshima; naye Sulemani mwanawe akatawala badala yake.
Lakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akachunguza, akatunga mithali nyingi.
Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa inakuja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba.