Mathayo 9:38 - Swahili Revised Union Version Basi mwombeni Bwana wa mavuno, atume wafanya kazi katika mavuno yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi mwombeni mwenye mavuno atume wafanyakazi wavune mavuno yake.” Biblia Habari Njema - BHND Basi mwombeni mwenye mavuno atume wafanyakazi wavune mavuno yake.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi mwombeni mwenye mavuno atume wafanyakazi wavune mavuno yake.” Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili atume watendakazi katika shamba lake la mavuno.” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo mwombeni Mwenyezi Mungu, Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno.” BIBLIA KISWAHILI Basi mwombeni Bwana wa mavuno, atume wafanya kazi katika mavuno yake. |
Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa vipawa katikati ya wanadamu; Naam, hata na wakaidi, BWANA Mungu akae nao.
nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu.
Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa BWANA, mfano wa manyunyu katika nyasi; yasiyowategemea watu, wala kuwangojea wanadamu.
Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawatuma ninyi.
Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yanakuja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.
Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.
Na Mungu ameweka wengine katika kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, aina za usaidizi, maongozi na aina za lugha.
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa kote kama ilivyo kwenu;