Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mika 5:7 - Swahili Revised Union Version

7 Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa BWANA, mfano wa manyunyu katika nyasi; yasiyowategemea watu, wala kuwangojea wanadamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Wazawa wa Yakobo watakaobaki hai wameenea miongoni mwa mataifa mengi, watakuwa kama umande wa Mwenyezi-Mungu uburudishao, kama manyunyu yaangukayo penye nyasi ambayo hayasababishwi na mtu wala kumtegemea binadamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Wazawa wa Yakobo watakaobaki hai wameenea miongoni mwa mataifa mengi, watakuwa kama umande wa Mwenyezi-Mungu uburudishao, kama manyunyu yaangukayo penye nyasi ambayo hayasababishwi na mtu wala kumtegemea binadamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Wazawa wa Yakobo watakaobaki hai, wameenea miongoni mwa mataifa na watu wengi watakuwa na nguvu kubwa kama simba kati ya wanyama wa porini, kama mwanasimba miongoni mwa makundi ya kondoo, ambaye kila mahali apitapo, huyarukia na kuyararua mawindo yake, asiwepo mtu yeyote wa kuyaokoa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Mabaki ya Yakobo yatakuwa katikati ya mataifa mengi kama umande kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kama manyunyu juu ya majani, ambayo hayamngoji mtu wala kukawia kwa mwanadamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Mabaki ya Yakobo yatakuwa katikati ya mataifa mengi kama umande kutoka kwa bwana, kama manyunyu juu ya majani, ambayo hayamngoji mtu wala kukawia kwa mwanadamu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa BWANA, mfano wa manyunyu katika nyasi; yasiyowategemea watu, wala kuwangojea wanadamu.

Tazama sura Nakili




Mika 5:7
40 Marejeleo ya Msalaba  

Hivyo tutamfikia mahali popote atakapoonekana, na kumwangukia kama vile umande uangukavyo juu ya nchi; wala hatutaacha hata mmoja wao, yeye na watu wote walio pamoja naye.


Watu wako watajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako.


Ni kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.


Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi.


Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani.


hata roho itakapomwagwa juu yetu kutoka juu; hata jangwa litakapokuwa shamba lizaalo sana; nalo shamba lizaalo sana litakapohesabiwa kuwa msitu.


Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;


Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;


Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa.


Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.


Lakini, tazama, watasalia mabaki watakaochukuliwa nje, wana na mabinti; tazama, watawatokea ninyi, nanyi mtaiona njia yao na matendo yao; nanyi mtafarijika katika habari ya mabaya niliyoleta juu ya Yerusalemu, naam, katika habari ya mambo yote niliyoleta juu yake.


Baadaye akanileta tena mpaka lango la nyumba; na tazama, maji yalitoka chini ya kizingiti cha nyumba, kwa njia ya mashariki, maana upande wa mbele wa nyumba ulielekea upande wa mashariki; nayo maji yakashuka toka chini ya upande wa kulia wa nyumba, upande wa kusini wa madhabahu.


Bwana MUNGU asema hivi; Huu ndio Yerusalemu; nimeuweka kati ya mataifa, na nchi zauzunguka pande zote.


Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.


Nitakuwa kama umande kwa Israeli; naye atachanua maua kama nyinyoro, na kuieneza mizizi yake kama Lebanoni.


Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.


Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA.


Yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni; yamkini kwamba BWANA, Mungu wa majeshi, atawafanyia fadhili mabaki ya Yusufu.


Hakika nitakukusanya, Ee Yakobo, nyote pia; Bila shaka nitawakusanya waliobaki wa Israeli; Nitawaweka pamoja kama kondoo katika zizi; Kama kundi la kondoo katika malisho yao; Watafanya mvumo kwa wingi wa watu;


Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utapondaponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa BWANA, na mali zao kwa BWANA wa dunia yote.


Nami nitamfanya yeye aliyechechemea kuwa mabaki, na yeye aliyetupwa mbali kuwa taifa lenye nguvu, na BWANA atawamiliki katika mlima Sayuni tangu sasa na hata milele.


Kwa sababu hiyo atawatoa, hata wakati wa kuzaa kwake aliye na uchungu; ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia wana wa Israeli.


Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa, kati ya kabila nyingi, mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwanasimba kati ya makundi ya kondoo, ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyagakanyaga na kuraruararua, wala hakuna wa kuokoa.


Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hadumishi hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema.


Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; wala ulimi wa hadaa hautakuwa kinywani mwao; kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewatisha.


Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba maji yaliyo hai yatatoka katika Yerusalemu; nusu yake itakwenda upande wa bahari ya mashariki, na nusu yake upande wa bahari ya magharibi; wakati wa joto na wakati wa baridi itakuwa hivi.


Maana nimejipindia Yuda, nimeujaza upinde wangu Efraimu; nami nitawachochea wana wako, Ee Sayuni, wapigane na wana wako, Ee Ugiriki, nami nitakufanya wewe kuwa kama upanga wa shujaa.


Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.


Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona ninyi wenyewe kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.


Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie.


Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.


Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema, Nilipatikana nao wasionitafuta, Nilidhihirika kwao wasioniulizia.


Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao?


Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani;


Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.


Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea.


Gideoni akamwambia Mungu, Ikiwa wewe utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo