Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.
Mathayo 9:29 - Swahili Revised Union Version Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu na itendeke kwenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyoamini.” Biblia Habari Njema - BHND Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyoamini.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyoamini.” Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Isa akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.” Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Isa akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.” BIBLIA KISWAHILI Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu na itendeke kwenu. |
Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.
Naye Yesu akamwambia yule afisa, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona wakati ule ule.
Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.
Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana.
Yesu akamwambia, Nenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.