Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,
Mathayo 8:1 - Swahili Revised Union Version Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu aliposhuka mlimani, makundi mengi ya watu yalimfuata. Biblia Habari Njema - BHND Yesu aliposhuka mlimani, makundi mengi ya watu yalimfuata. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu aliposhuka mlimani, makundi mengi ya watu yalimfuata. Neno: Bibilia Takatifu Isa aliposhuka kutoka mlimani, makundi ya watu wakamfuata. Neno: Maandiko Matakatifu Isa aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata. BIBLIA KISWAHILI Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. |
Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,
Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya;
Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Yudea, na ng'ambo ya Yordani.
Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.
Naye Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake, akaenda baharini. Mkutano mkuu ukamfuata, kutoka Galilaya, na Yudea,
Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao.