Mathayo 6:21 - Swahili Revised Union Version kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako pia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako. Biblia Habari Njema - BHND Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako. Neno: Bibilia Takatifu Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo pia moyo wako utakapokuwa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo pia moyo wako utakapokuwa. BIBLIA KISWAHILI kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako pia. |
Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.
Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia, na kudhulumu, na kutenda jeuri.
Ee Yerusalemu, jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini?
Enyi wazawa wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.
Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.
tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakudai hata nafsi yako.
Hadharini, ndugu zangu, usiwepo katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutoamini, ujitengao na Mungu aliye hai.