Mathayo 5:5 - Swahili Revised Union Version Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Heri walio wapole, maana watairithi nchi. Biblia Habari Njema - BHND Heri walio wapole, maana watairithi nchi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Heri walio wapole, maana watairithi nchi. Neno: Bibilia Takatifu Heri walio wapole, maana hao watairithi nchi. Neno: Maandiko Matakatifu Heri walio wapole, maana hao watairithi nchi. BIBLIA KISWAHILI Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. |
Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.
bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.
Wanyenyekevu nao wataongeza furaha yao katika BWANA, na maskini katika wanadamu watafurahi katika Mtakatifu wa Israeli.
Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, Nao watairithi nchi milele; Wao ni chipukizi nililolipanda mimi mwenyewe, Kazi ya mikono yangu mwenyewe, Ili mimi nitukuzwe.
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.
Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda, Na mwanapunda, mtoto wa punda.
Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Abrahamu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa imani.
Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,
Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, subira, upole.
akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awajalie ili watubu na kuijua kweli;
Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Ni nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aoneshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa heshima.
bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.