Basi sasa, tengenezeni njia zenu, na matendo yenu, mkaisikilize sauti ya BWANA, Mungu wenu; naye BWANA atayaghairi mabaya aliyoyanena juu yenu.
Mathayo 3:8 - Swahili Revised Union Version Basi zaeni matunda yapasayo toba; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Onesheni kwa vitendo kwamba mmetubu. Biblia Habari Njema - BHND Onesheni kwa vitendo kwamba mmetubu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Onesheni kwa vitendo kwamba mmetubu. Neno: Bibilia Takatifu Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. Neno: Maandiko Matakatifu Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. BIBLIA KISWAHILI Basi zaeni matunda yapasayo toba; |
Basi sasa, tengenezeni njia zenu, na matendo yenu, mkaisikilize sauti ya BWANA, Mungu wenu; naye BWANA atayaghairi mabaya aliyoyanena juu yenu.
Huenda nyumba ya Yuda watasikia mabaya yote niliyokusudia kuwatenda; wapate kurudi, kila mtu akaiache njia yake mbaya; nami nikawasamehe uovu wao na dhambi yao.
Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Abrahamu watoto.
bali kwanza niliwahubiria wale wa Dameski na Yerusalemu, na katika nchi yote ya Yudea, na watu wa Mataifa, kwamba watubu na kumwelekea Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.
Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; nendeni kama watoto wa nuru,