Mathayo 28:4 - Swahili Revised Union Version Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walinzi wa lile kaburi wakatetemeka kwa hofu kubwa, hata wakawa kama wamekufa. Biblia Habari Njema - BHND Walinzi wa lile kaburi wakatetemeka kwa hofu kubwa, hata wakawa kama wamekufa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walinzi wa lile kaburi wakatetemeka kwa hofu kubwa, hata wakawa kama wamekufa. Neno: Bibilia Takatifu Wale walinzi wa kaburi walimwogopa sana, wakatetemeka hata wakawa kama wafu. Neno: Maandiko Matakatifu Wale walinzi wa kaburi walimwogopa sana, wakatetemeka hata wakawa kama wafu. BIBLIA KISWAHILI Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. |
Nami, Danieli, nikaona maono haya peke yangu; maana wale watu waliokuwa pamoja nami hawakuyaona maono haya; lakini tetemeko kuu liliwashika, hata wakakimbia ili kujificha.
Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya walinzi waliingia mjini, wakawaambia wakuu wa makuhani juu ya mambo yote yaliyotendeka.
Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa.
Nami nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,