Mathayo 28:3 - Swahili Revised Union Version Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alionekana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. Biblia Habari Njema - BHND Alionekana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alionekana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. Neno: Bibilia Takatifu Sura ya huyo malaika ilikuwa kama umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. Neno: Maandiko Matakatifu Sura ya huyo malaika ilikuwa kama umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. BIBLIA KISWAHILI Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji. |
Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.
akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
Wakaingia kaburini wakaona kijana akiwa ameketi upande wa kulia, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu.
Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu.
Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,
Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.
Baada ya hayo niliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, akiwa na mamlaka makuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.